Yanga wampigia magoti Zahera | Bingwa

Yanga wampigia magoti Zahera | Bingwa. Apply Here for this job.

Yanga wampigia magoti Zahera | Bingwa. See full details below.

HUSSEIN OMAR

WACHEZAJI wa zamani wa Yanga wakiongozwa na Sunday
Manara, wamepanga kukutana na kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, kwa ajili
ya kumwomba msamaha kutokana na madudu ya usajili yaliyofanywa na viongozi wa klabu
hiyo.

Akizungumza na BINGWA jana, Mwenyekiti wa Umoja wa
Wachezaji wa zamani wa Yanga, Ramadhan Kampira, alisema wamefedheheshwa na
kitendo cha udanganyifu kilichofanywa na Kamati ya Usajili iliyo chini ya
Mwenyekiti wake, Hussein Nyika.

Kamati hiyo ilishindwa kuwasajili wachezaji
waliopendekezwa na kocha huyo ili kuimarisha kikosi wakati wa usajili wa
dirisha dogo kabla  halijafungwa hivi
karibuni.

Miongoni mwa wachezaji ambao Yanga wameshindwa
kuwasajili ni pamoja na golikipa wa Tanzania Prisons, Aron Kalambo, winga raia
wa Ureno mwenye asili ya DR Congo, Reuben Bemba, straika wa Mwadui FC, Charles
Ilamfya na Eliud Ambokile.

Kampira alisema wamefedheheshwa na kitendo hicho
hivyo wamepanga kuonana na Zahera ili 
kumwomba msamaha kutokana na madudu hayo yaliyofanyika.

“Wameidhalilisha Yanga kwa kweli kitendo  walichokifanya si kizuri, hata mwalimu pia
atatudharau sisi katika jambo hili ndiyo maana tumepanga kumwomba msamaha kwa
niaba ya Wanayanga,’’ alisema Kampira.

Aidha, alieleza kuwa walichokifanya viongozi hao ni
kinyume na maadili ya mpira wa miguu, hivyo wanaendelea kuwafuatilia kwa karibu
na endapo itagundulika walifanya udanganyifu watawapeleka mbele ya vyombo vya
dola.

“Bado tunaendelea kuwafuatilia na ikibainika kuna
vitendo vya halali vilifanyika tutakwenda mbele ya sheria ili iwe fundisho kwa
wengine,’’ alisema Kampira.

Tangu kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf
Manji, Mei mwaka jana, mambo yanakwenda ndivyo sivyo ndani ya Yanga kutokana na
viongozi walioachiwa jahazi kushindwa kutimiza baadhi ya majukumu.For latest info, Click Here

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here