Yanga hawaachi kitu | Bingwa

Yanga hawaachi kitu | Bingwa. Apply Here for this job.

Yanga hawaachi kitu | Bingwa. See full details below.

*Baada ya kukaa kileleni Ligi Kuu, walitaka Kombe la Shirikisho kwa kuichapa Tukuyu Stars

WINFRIDA MTOI

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga,
wameonyesha kuwa wamepania kufanya kweli msimu huu baada ya kuichapa Tukuyu
Stars mabao 4-0 katika mchezo wa Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Yanga walitoa dozi hiyo kwa Tukuyu Stars
katika mchezo wa jana uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Wakati Yanga wakishinda mchezo huo na kutinga
hatua ya 32 bora, mshambuliaji wao, Amiss Tambwe, alipiga ‘hat-trick’, huku
lile la nne likifungwa na Heritier Makambo.

Katika mchezo huo ambao Yanga walimtumia
kwa mara ya kwanza mchezaji wao mpya, Haruna Moshi ‘Boban’ aliyejiunga kutoka
African Lyon, ulianza kwa kasi na Amis Tambwe kupachika bao la kwanza dakika ya
13, kisha dakika tano baadaye Makambo alikosa bao dakika ya 18 baada ya
kutengewa pasi nzuri na Ibrahim Ajib.

Dakika nane baadaye naye Tambwe alikosa
bao kwa kupaisha mpira juu alipotaka kuunganisha pasi ya Boban ambaye
alipumzishwa dakika ya 29, baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Deus
Kaseke.

Tambwe alifunga bao la pili dakika ya 37,
akiunganisha kwa kichwa mpira uliopigwa na Kaseke na Yanga kwenda mapumziko
wakiongoza kwa mabao 2-0.

Timu hizo zilirudi kipindi cha pili na
kushambuliana na dakika ya 55, Tambwe aliwapita mabeki wa Tukuyu na kufunga bao
la tatu, kisha Makambo kuongeza la nne dakika ya 80.

For latest info, Click Here” byFor latest info,
Click Here

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here